JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2015/16
JIHADHARI NA MATAPELI
Kumekuwepo
na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16
(TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii.
Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara
haihusiki nazo.
Aidha,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa
ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka
Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.
Kutokana na
mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira
mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka
inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara watakapokamilisha
taratibu zinazotakiwa.
Chanzo:chingaone.com
Harrah's Cherokee Casino & Hotel - Mapyro
ReplyDeleteGet directions, reviews and information 문경 출장마사지 for Harrah's Cherokee Casino & Hotel in Cherokee, NC. 여수 출장샵 The 구미 출장마사지 hotel has a 2,200 보령 출장마사지 room luxury hotel, located in the resort's 시흥 출장안마